14 Septemba 2026 - 11:10
Walinzi wa Mapinduzi: Tumeiangamiza ndege isiyo na rubani ya MQ-1 juu ya Mlango Bahari wa Hormuz

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran limesema mfumo wake wa ulinzi wa anga umefanikiwa kuikamata na kuiangamiza ndege ya kisasa isiyo na rubani aina ya MQ-1 iliyokuwa ikiruka juu ya Mlango Bahari wa Hormuz.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuiangamiza ndege ya kisasa isiyo na rubani aina ya MQ-1 juu ya Mlango Bahari wa Hormuz.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA), likinukuu tovuti ya habari ya IRGC, mfumo wa ulinzi wa anga wa Walinzi wa Mapinduzi uliweza kuikamata na kuiangamiza ndege hiyo isiyo na rubani baada ya kugunduliwa na mtandao jumuishi wa ulinzi wa anga wa Iran.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya kimkakati inayounganisha Ghuba ya Uajemi na Ghuba ya Oman.

Aidha, Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi lilitangaza katika taarifa yake ya awali ya 10 Septemba kwamba lilifanikiwa kuishambulia ndege nyingine ya adui isiyo na rubani yenye namba 5838, aina ya Sea-Drone, katika lango la Mlango Bahari wa Hormuz na kuzuia kutekelezwa kwa dhamira yake ya kichokozi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha